Bongo Fc


Mo awageukia wachezaji simba

Mshindi wa zabuni ya ununuzi wa hisa za Klabu ya Simba, Mohamed "MO" Dewji , amewataka wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa kujituma na kutambua thamani ya kuvaa jezi ya klabu hiyo.

Dewji, alisema Simba ni klabu kubwa na wachezaji wanaopata nafasi ya kuichezea wanapaswa kujituma na kuonyesha uwezo unaoendana na jina la klabu hiyo.

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Dewji, alisema kuwa kama wachezaji watapambana uwanjani na kujituma, wananafasi kubwa ya kuiletea timu hiyo mafanikio.

“Simba ni timu kubwa, nimekuwa shabiki wa timu hii tangu nikiwa mtoto, nilipanga kwa miaka mingi lazima nije kuisadia timu hii, wachezaji wetu wanapaswa kutambua thamani ya kuvaa jezi ya timu hii, ni lazima wajitume uwanjani ili kuipa mafanikio,” alisema Dewji.

Aidha, alisema atakuwa karibu na wachezaji kuhakikisha wanaitumikia klabu hiyo katika mazingira mazuri yatakayowafanya kujituma uwanjani.

“Mambo yakishakamilika (taratibu za kubadili mfumo wa uwendeshwaji), Simba haitakuwa timu ya kuwania ubingwa wa ndani pekee, itakuwa timu ya kuwania ubingwa wa Afrika na kushindana na timu nyingine kubwa Afrika,” aliongeza kusema.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.