Bongo Fc


Bayern munich yajitwisha kibarua kizito kuipiku psg

Bayern Munich licha ya kuwa nyumbani leo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya PSG ambayo wanakutana leo, huku timu hiyo ya Ujerumani ikitakiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4 dhidi ya wapinzani wao kama wanataka kuwa kinara kwenye Kundi B.

PSG inaongoza kundi B ikiwa na pointi 15 huku ikifuatiwa na Bayern Munich yenye pointi 12. Mchezo wa leo utaipa nafasi timu hiyo ya Bundersliga kusonga mbele hata kama wasiposhinda lakini iwapo itafanikiwa kushinda mabao manne, watavuka wakiwa vinara wa kundi hilo.

Ushindi wa awali wa PSG kwenye mchezo uliofanyika mwishoni mwa Septemba, uliwaweka nafasi nzuri na kukaa kileleni kwenye kundi hilo, huku Wajerumani hao wakitakiwa kupambana ili kulipa kisasi kwa kuhakikisha wanapata mabao manne.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.