Bongo Fc


Liverpool yapiga hesabu kufuzu 16 bora

Liverpool inajitupa kesho Jumatano uwanjani kukamilisha mchezo wa mwisho wa makundi ambapo itakutana na Spartak Moscow, huku ikihitaji sare tu kujihakikishia kutinga hatua ya 16 bora.

Liverpool imejiweka kileleni baada ya kukusanya pointi 9 na ikifuatiwa na Sevilla yenye pointi 8 katika nafasi ya pili.

Vita ya kutinga hatua ya 16 bora pia imeikumba klabu ya Spartak Moscow ambayo ushindi wowote itaiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu iwapo tu Sevilla itatoka sare.

Liverpool ipo kwenye hatari ya kukosa kuwa kileleni kwenye kundi lakini bado ina nafasi ya kuvuka kwenda hatua ya 16 bora.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.