Bongo Fc


Atupele green aziita klabu mezani

Siku chache baada ya kutupiwa virago aliyekuwa mshambuliaji wa Singida United, Atupele Green, ameziita klabu zinazohitaji huduma yake mezani na kufanya mazungumzo.

Jumatatu klabu ya Singida ilitangaza kuachana na wachezaji wake watatu, akiwamo mshambuliaji huyo waliyemsajili Mei mwaka huu akitokea JKT Ruvu iliyoshuka daraja, yakiwa ni matakwa ya kocha Hans Van der Pluijm.

Atupele hadi anatupiwa virago alikuwa hajafanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao, katika mabao matano yaliyofungwa na timu ndani ya michezo 11 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi, Atupele alisema mchezaji kuachwa katika timu ni kitu cha kawaida, anachokifanya ni kuzikaribisha klabu nyingine kufanya naye mazungumzo kwani bado ana uwezo wa kupambana uwanjani kutimiza jukumu lake hilo la kufunga.

“Sichagui timu ya kuchezea kikubwa ni makubaliano katika mkataba wa pande zote mbili, klabu ambayo iko tayari tuonane, mpira ndio kazi yangu yaliyopita yamepita tugange yajayo,” alisema.

Nyota huyo aliyewahi kuichezea Ndanda ya mkoani Mtwara, miongoni mwa mafanikio aliyoyapata katika soka ni kutwaa kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa Kombe la Azam Sports Federation msimu wa 2015/16.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.