Bongo Fc


Fahamu ofa aliyoikataa messi kisa kubaki barca

Unaambiwa Lionel Messi aliikataa ofa nono ya mkataba wenye nyongeza ya pauni milioni 88 za dili la uhamisho kutoka Manchester City na kuamua kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika viunga vya Barcelona.

Muargentina huyo alimaliza utata wa hatima yake ndani ya dimba la Nou Camp mapema mwezi uliopita kwa kusaini mkataba huo mpya utakaomfanya alipwe mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki hadi 2021.

Lakini kwa mujibu wa mtandao wa Marca, Messi alifikia huko baada ya Man City kujaribu kumshawishi na ofa ya maana ambayo hata hivyo Messi aliipiga chini.

Inasemekana kuwa City walimtamanisha na dili la kuwa wangemlipa mshahara wa pauni 850,000 kwa wiki sambamba na nyongeza nyingine ya kukubali kuhamia England tu.

Marca waliendelea kudai kuwa mawakala wa Messi walifuatwa na vinara hao wa Ligi Kuu England bila ruhusa maalumu kutoka kwa Barca.

City waliwahi mapema sana kwani Messi angeweza kukaa mezani na kuanza mazungumzo na City Januari mwakani kama asingekuwa amesaini mkataba mpya. Mkataba wake wa zamani ulikuwa unatarajiwa kumalizika majira yajayo ya kiangazi.

City walitambua wazi kuwa njia nyepesi ya kumnasa Messi ni kumuwahi sasa hivi na si kusubiri tena. Lakini mwisho wa siku Messi hakushawishika kutoka kwa vinara wa La Liga kwenda kwa Ligi Kuu England.

Barcelona wanaendelea kushikilia usukani wa La Liga kwa tofauti ya pointi tano baada ya kuanza msimu bila kufungwa katika ligi yao hiyo. Messi mwenyewe hadi sasa ametupia mabao 13 katika mechi 14 za ligi msimu huu chini ya kocha Ernesto Valverde.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.