Bongo Fc


Z'bar heroes yaifuata kenya kibabe fainali

Zanzibar Heroes imetinga fainali ya Kombe la Chalenji kibabe kwa kuwavua ubingwa Uganda kwa kuichapa kwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya pili iliyofanyika kwenye Uwanja wa Moi, Kisumu, Kenya.

Katika mchezo huo mabao ya Zanzibar yalifungwana Abdulaziz Makame dakika 7, penalti ya Mohammed Issa 'Banka' dakika 54, huku bao la kufutia machozi kwa Uganda likifungwa na Nsibambi Derrick.

Ushindi huo ni kuelendeleza rekodi nzuri ya Zanzibar katika mashindano ya mwaka huu na sasa inajiandaa na fainali ya Jumapili dhidi ya wenyeji Kenya ikiwa ni marudiano ya mechi ya hatua ya makundi iliyomalizika kwa suluhu.

Timu hiyo ilianza mchezo huo taratibu na kuonekana kuzidiwa kwa kiasi kikubwa umiliki wa mpira kipindi cha kwanza, lakini kadri muda ulivyoenda walibadilika na kucheza kwa kiwango cha juu.

Uzembe wa mabeki wa Uganda kushindwa kuokoa kona mpira huo ulimkuta Abdulaziz Makame wa Zanzibar akiwa pembeni na kupiga shuti huku akiwacha mabeki watano wa Uganda waliokuwa golini wakishangaa.

Bao hilo halikuidumu muda mrefu kwani dakika sita baade Uganda walisawazisha kupitia kwa Nsibambi Derrick kwa shuti kali akimalzia pasi ya Kyambadde Allan.

Timu hizo zilienda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1 na kipindi cha piliu Zanibar ilirejea kwa nguvu zaidid na kuonekana imepania kutinga nusu fainali.

Dakika ya 54, Zanzibar Heroes ilifanya shambulizi la kushtukiza kupitia Ibrahim Ahmada akielekea kufunga beki wa Uganda, Nsubuga Joseph alimvuta jezi na kuanguka katika eneo la penalti na mwamuzi,Twagirumukiza wa Rwanda kuamuru Penalti huku pia akimzawadia beki huyo kadi nyekundu.

Mohammed Issa'Banka' aliipatia Zanzibar Heroes bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 57 na kuamsha nderemo kwa wachezaji na mashabiki wa timu hiyo.

Pamoja na Uganda kuwa pungufu bado waliendelea kulisakama lango la Zanzibar lakini mabeki na kipa wa Heroes walikuwa makini kuokoa hatari hizo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo 2-1.

Uganda bingwa wa kihistori atacheza mechi ya mshindi wa tatu dhidi ya Burundi Jumapili mapema kabla ya Kenya kuivaa Zanzibar katika fainali siku hiyo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.