Bongo Fc


Iniesta adai haitapendeza neymar kwenda real

Kiungo mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta amesema hana hofu kuhusu Neymar kujiunga na Real Madrid lakini akakiri kuwa ikitokea hivyo haitampendeza kutokana na uhusiano wa Neymar na mastaa wengine wa Barcelona wakati alipokuwa akiichezea timu hiyo.

Iniesta amecheza na Neymar kwa miaka minne kabla ya mchezaji huyo kuondoka na kuhamia Paris Saint- Germain lakini kumekuwa na taarifa za kuwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid.

“Chochote kinaweza kutokea kwenye soka, kuna mambo ambayo yalionekana ni vigumu kutokea na yakatokea, sitashangaa lakini haitapendeza kwa kuwa kwa kuwa ni mchezaji mzuri lakini sina hofu,” alisema Iniesta.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.