Bongo Fc


Msuva asikitishwa na stars kufanya vibaya challenge

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayechezea klabu ya Difaa Hassan El- Jadida ya Morocco, amesikitishwa na matokeo mabaya ya timu ya Tanzania Bara katika michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya.

Msuva amesema kuwa amesikitishwa sana na matokeo hayo, kwani kwa kiasi kikubwa wachezaji wanaokuwa kwenye kikosi cha Bara ndiyo huunda Taifa Stars.

“Ukitazama kikosi cha Challenge sana sana tumekosekana mimi, Banda (Abdi) na Kapteni wetu (Mbwana Samatta) ili kuwa Taifa Stars, maana yake hiyo ndiyo timu inayotegemewa kwa kampeni za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Kwa kweli ni mbaya sana,”amesema Msuva.

Hata hivyo, mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, amesema kwamba watajipanga upya baada ya matokeo hayo ya kusikitisha ili warejeshe heshima.

Msuva amewataka Watanzania kutokata tamaa na timu yao, bali kuendelea kuiunga mkono, kwani iko siku mambo yatakuwa mazuri.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.