Bongo Fc


Matola adai hazihofii simba, yanga kwasi akisepa

Kocha wa Lipuli ya Iringa, Suleiman Matola, amesema hana hofu ya kikosi chake kuendelea kuzisumbua klabu za Simba na Yanga watakapokutana tena.

Matola ambaye alikuwa nahodha na kocha msaidizi wa zamani wa Simba ameiambia BongoFC kuwa, anazifahamu vizuri klabu hizo kubwa na anajua mapungufu yao.

“Hata kama nitakutana na timu hizi kesho tutaendelea kuwasumbua, nafahamu udhaifu wao,” alisema Matola. Aidha, aligusia kuwa kuondoka kwa beki wake kisiki, Asante Kwasi anayewaniwa na Simba hakutaifanya timu hiyo kupoteza makali yake.

“Kwasi ni mchezaji mzuri na ndio maana timu zinamgombania, lakini niseme tu Lipuli tuna wachezaji wengi kwenye nafasi yake, wala haitakuwa shida sana akiondoka kwa sababu wapo watakaoziba nafasi yake,”alisema Matola.

Inaelezwa Simba wapo kwenye hatua za mwisho kumsajili beki huyo raia wa Ghana ambaye amekuwa kikwazo kwa washambuliaji wa klabu hizo kubwa nchini.

Lipuli haijafungwa na Simba na Yanga zinazodhaminiwa kwa sasa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kwenye mechi zake za Ligi Kuu walizocheza katika Uwanja wa Uhuru baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.