Bongo Fc


Gwiji wa brazil, ricardo kaka atangaza rasmi kustaafu soka

Mwanasoka nyota wa Brazil, Ricardo Izecson dos Santos Leite 'Kaka' ametangaza rasmi kustaafu.

Kaka mwenye umri wa miaka 35 sasa, msimu uliopita alichezea Orlando City ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) na alisema atastaafu mwishoni mwa msimu.

Mbrazil huyo alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Colombus Crew mwezi Oktoba - mchezo ambao timu yake ilifungwa 1-0.

Tangu hapo haikuwekwa wazi kama Kaka atarudi kucheza mechi moja ya kuaga na timu yake ya taifa, Brazil, au atastaafu moja kwa moja mchezo alioupenda maishani mwake.

Lakini jana ameposti kwenye mtandao wa kijamii kuweka wazi hilo. Aliposti picha yake isiyo ya rangi akiwa amevaa fulana yake maarufu 'Mimi ni wa Yesu' aliyoionyesha kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, Kaka ametoa taarifa juu ya mustakabali wake.

'Baba, Ilikuwa zaidi ya nilivyofikiria. Nakushukuru! Sasa niko tayari kwa safari nyingine. Katika jina la Yesu. Amin,"ameandika Kaka.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.