Bongo Fc


Mourinho aivuruga barcelona

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amedaiwa kuwa katika mipango kabambe ya kutaka kuwasajii nyota wawili wa Barcelona, Samuel Umtiti na Sergi Roberto.

Habari zinasema kuwa kocha huyo raia wa Ureno anadhani watu hao watasababisha timu yake iwe na ushindani mkubwa kuanzia Januari. Habari zinasema kuwa Roberto anaweza kupatikana kwa kiasi cha Pauni 35milioni na jambo hilo linaongeza uwezekano wa kutua katika klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

Suala la kuchukua ubingwa katika Ligi Kuu England msimu huu linaonekana kuwa gumu lakini kocha huyo hakati tamaa na anadhani kwamba kama wakishindwa kunyanyua ndoo basi washike nafasi ya pili.

Licha ya kutumia pesa nyingi kuwasajili nyota kama Romelu Lukaku na Nemanja Matic, katika dirisha la usajili lililopita, kocha huyo bado anaona nguvu iliyopo si ya kutisha sana.

Umtiti atakuwa mwiba katika safu ya ukabaji Roberto akionekana kuwa suluhisho katika nafasi ya kiungo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.