Bongo Fc


Wilshere, sturridge, draxler kupigwa bei

Jack Wilshere, Daniel Sturridge na Julian Draxler ni miongoni mwa majina ya wachezaji nyota 10 wanatakiwa kuzihama klabu zao katika dirisha dogo la usajili Januari, mwakani.

Wachezaji hao wanatakiwa kuzihama klabu zao kama wana ndoto ya kuzitumikia timu za Taifa katika fainali za Kombe la Dunia zilizopangwa kuchezwa mwakani Russia.

Nyota hao hawana namna zaidi ya kuondoka baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza. Makocha wa timu za Taifa wako ‘msituni’ kuangalia wachezaji wenye viwango bora.

Baadhi ya nyota wengine wanatakiwa kuhama Mbelgiji Michy Batshuayi aliyekosa namba Chelsea. Luke Shaw Manchester United na Danny Rose wa Tottenham Hotspurs wanaocheza nafasi ya beki wa kushoto katika kikosi cha England.

Fainali hizo zimebakiza takribani miezi mitano kabla ya kuanza kutimua vumbi na kila timu inatakiwa na wachezaji 23 watakaokwenda Russia.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.