Bongo Fc


Juventus: paul dybala haondoki chini ya paundi milioni 133

Imeripotiwa kuwa Juventus imeiambia Manchester United kuwa Paulo Dybala haondoki bila paundi milioni 133.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa kwenye kiwango bora duniani tangu ajiunge na Bianconeri kutoka Palermo mwaka 2015.

Dybala ana magoli 57 na pasi za magoli 22 katika mechi 119 akiwa na Juve hadi sasa na imeisaidia klabu hiyo kutetea taji la Serie A na Coppa Italia mfululizo.

Kwa mujibu wa Calciomercato, Jose Mourinho anamuona Dybala kama mrithi wa muda mrefu wa Zlatan Ibrahimovic, lakini Mashetani wekundu hao wameambiwa kuwa thamani ya nyota huyo si chini ya paundi milioni 133.

Dybala pia amekuwa akiwindwa na Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich.

Manchester United imetenga zaidi ya paundi milioni 200 kwenye dirisha lijalo la usajili kwa ajili ya kukisuka upya kikosi chao, majina kadhaa yamekuwa yakiorodheshwa kujiunga na United kama Dyabala, Malcom, Bale na wengineo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.