Bongo Fc


Mahrez ataka kumrithi sanchez

Wakati Alexis Sanchez akitarajiwa kujiunga na kikosi cha Manchester City Januari hii kutoka Arsenal, nyota wa Algeria anayekipiga katika kikosi cha Leicester City, Riyad Mahrez, amesema anataka kuchukua nafasi ya Sanchez ndani ya The Gunners.

Mahrez ameviambia vyombo vya habari nchini England kwamba yeye yupo tayari kujiunga na Arsenal katika usajili wa dirisha dogo, kwa sababu ni moja ya matamanio yake kama mchezaji kucheza kwenye timu kubwa.

“Tamaa yangu kama mchezaji ni kucheza katika klabu kubwa kama Arsenal, naamini kwamba nafasi ya Sanchez naweza kuichukua iwapo akijiunga na Manchester City ya England,” amesema Mahrez.

Jambo hilo huenda likawa kwenye nafasi bora zaidi baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba klabu ya Arsenal inatarajia kutenga kiasi cha Euro milioni 44 ili kupata saini ya Mahrez mwenye umri wa miaka 26.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.