Bongo Fc


Wenger adai penalti ya chelsea ni kichekesho

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameonyesha jazba yake kuhusu Chelsea kupewa penalti Jumatano usiku katika mechi za Ligi ya Uingereza.

Mechi hiyo iliishia kwa sare ya 2-2 kwa Gunners, shukrani kwa Hector Bellerin aliyeweka kimiani dakika za lala salama.

Arsenal walifungua ukurasa wa mabao kwa goli la Jack Wilshere baada ya saa moja ya mchezo, lakini ndani ya dakika nne tu baadaye, Eden Hazard alisawazisha kwa mkwaju wa penalti.

Wenger alihisi mwamuzi amekosea kupuliza kipyenga baada ya Hazard kuanguka kufuatia changamoto kutoka kwa Bellerin.

"Nilidhani ni mechi nzuri yenye mvuto. Tulionyesha uwezo wetu wa kutumia akili," Mfaransa huyo aliwaambia waandishi. "Uamuzi wa kutoa penalti ile ulikuwa kichekesho kweli. Sitaki kuizungumzia, Nimechoka.

"Ni budi tujiandae na kile ambacho tunakabiliana nacho," Wenger alisema kupitia BBC Sport. "Unatazma soka safi. Na kwa bahati mbaya unaona maamuzi mabaya.

"Sitaki kuanza [kuzungumzia maamuzi binafsi] kwa sababu yanakera na kukarahisha. [penalti ya Hazard] haikustahili."

Marcos Alonso aliifungia Chelsea na kufanya matokeo kuwa 2-1 mnamo dakika ya 84 kabla ya Bellerin kusawazisha.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.