Bongo Fc


Hazard: chelsea ilipaswa kuifunga arsenal

Nyota wa Chelsea Eden Hazard amedai kuwa timu yake ilipaswa kupata pointi zote tatu katika mechi ya ugenini dhidi ya Arsenal Jumatano usiku [Jana].

The Blues walifanikiwa kuongoza kwa 2-1 wakitokea nyuma baada ya kutangulia kufungwa, lakini goli la dakika ya 92 kutoka kwa Hector Bellerin liliumaliza mchezo huo kwa sare ya 2-2.

Hazard ndiye aliyesawazisha goli la kwanza la Jack Wilshere kipindi cha pili baada ya kupewa penalti, ambayo Arsene Wenger aliita "kichekesho".

"Ilikuw mechi ya 50-50, timu zote zimecheza mchezo mzuri sana," Hazard aliiambia Sky Sports News. "Huenda tungekuwa tumefunga zaidi, lakini tulikosa nafasi kadhaa. Yote yangekuwa magoli. Tunafurahi hata hivyo.

"Hatuhitaji kurudia video - ilikuwa penalti. Petr [Cech] ni kipa mahiri, ni vigumu mara zote kumfunga lakini niliukwamisha mpira wavuni na hilo ndilo jambo la msingi. Nadhani tulipaswa kushinda mechi hii kwa sababu ya nafasi tulizopata."

The Blues wanabakia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League, pointi moja nyuma ya Manchester United inayoshika nafasi ya pili.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.