Bongo Fc


Man united yajawa na hofu juu ya kocha wake jose mourinho

Vigogo wa Manchester United inaaminika wameanza kupata hofu kuwa Jose Mourinho atajiuzulu kama meneja ifikapo mwisho wa kampeni hizi.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea amekuwa katika kipindi kigumu wiki za hivi karibuni baada ya timu yake kujikuta nyuma ya Manchester City kwa pointi 15 katika mbio za ubingwa na ameweka bayana hadharani kuwa United hawajatumia fedha za kutosha kuwa washindani.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Kocha huyo wa miaka 54 "amezidi kujitenga, na kutumia muda mchache zaidi ya kawaida Manchester" katika kipindi cha hivi karibuni.

Mourinho ana nyumba ya familia London na anakaa kwenye hoteli anapokuwa akifanya kazi Manchester, lakini "amekuwa na safari nyingi kwenda kusini" ameamsha walakini kwenye akili za United wakijiuliza kwa nini hajahamia Manchester moja kwa moja.

Miezi miwili iliyopita Paris Saint-Germain ya Ligue 1 ambayo inatumia fedha nyingi kwa usajili ilisadikiwa kujiandaa kuonana na Mourinho, ambaye amebakiwa na miezi 18 kwenye mkataba wake wa sasa Old Trafford.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.