Bongo Fc


Huyu wenger vipi? atishia kujinyonga angefungwa na chelsea

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametishia kujinyonga iwapo kikosi chake kingefungwa na Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu jana Jumatano.

Mechi hiyo iliisha kwa sare ya mabao 2-2 huku Wenger akisema kwamba iwapo Chelsea wangebebwa tena kwa namna yote ile kisha kuibuka na ushindi angejinyonga hadi kufa.

Wenger alibainisha kwamba uamuzi wa kuipa Chelsea penalti na kupata sare ya 2-2 kwa upande wake anaona jambo hilo halikuwa sahihi.

Mwamuzi wa mchezo huo, Anthony Taylor hakusita kutoa adhabu ya penalti baada ya Eden Hazard kuchezewa vibaya na Hector Bellerin.

Alisema penalti hiyo iliwaathiri kwa kiasi kikubwa kwa sababu kulikuwa na mazingira a kuelekea kupoteza mechi hiyo huku akisema kwa maamuzi ya aina hiyo mwamuzi anaweza kujikuta anagawa hata penalti 10 kwenye mechi moja.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.