Bongo Fc


Mfumo wa kocha simba komesha

Ndani ya muda mfupi tu mashabiki wa Simba wameshamsahau aliyekuwa Kocha Mkuu wao, Joseph Omog, kutokana na kandanda safi linaloonyeshwa na kikosi chao chini ya mwalimu Masoud Djuma raia wa Burundi.

Djuma ambaye kwa sasa ni kaimu kocha mkuu, anapigiwa debe na mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao ili kukabidhiwa moja kwa moja timu kutokana na kuridhishwa na kazi nzuri anayoifanya, akiiongoza timu hiyo kupata matokeo mazuri kwenye baadhi ya mechi.

Simba chini ya Djuma, imeonekana kuimarika sana kupitia mfumo wa 3-4-3 na wakati mwingine 3-5-2 anayotumia kocha huyo ambayo huwa inatumiwa na baadhi ya makocha maarufu duniani, akiwamo Atonio Conte wa Chelsea ya England.

Tangu Djuma akabidhiwe timu baada ya kutemwa kwa Omog, amebadilisha mfumo wa uchezaji wa timu hiyo na kuifanya kucheza kwa kasi zaidi, huku akitumia zaidi mfumo mgumu wa 3-4-3 ambao makocha kadhaa hapa nchini waliushindwa.

Katika michezo aliyoiongoza timu hiyo, kocha huyo anaonekana kuwa na msimamo na mfumo huo licha ya vijana wake kupata shida kuutumia, lakini kwa sasa umeanza kumletea matunda mazuri.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, ni muumini wa mfumo huo ambao ulimpatia ubingwa msimu uliopita, huku kwa kiasi kikubwa ukihitaji wachezaji wa pembeni ‘wing-back’ .


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.