Bongo Fc


Hatimaye barcelona yamng’oa coutinho england

Mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho amekamilisha uhamisho wa kwenda Barcelona uliogharimu Pauni 150 milioni ikiwa ni rekodi mpya kwenye Ligi Kuu England na klabu ya Liverpool.

Mchezaji huyo alikwenda Hispania jana kwa ajili ya vipimo kabla ya kusaini mkataba ambao ndiyo atakuwa amekamilisha ndoto zake za kuhamia Nou Camp.

Hata hivyo, tayari Barcelona imethibitisha kumsajili nyota huyo wa Liverpool kwa mkataba huo mnono ambao unakaribia dau la usajili la mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr.

Miamba hao wa La Liga jana Jumamosi walitangaza kuhitimisha safari ya muda mrefu ya kumhitaji Coutinho ambaye ni raia wa Brazil.

Mchezaji huyo anatarajia kudondoka wino kwa ajili ya mkataba wa miaka mitano klabuni hapo Hispania.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.