Bongo Fc


Barca yamtangaza coutinho camp nou

Vinara hao wa La Liga wamemtambulisha mchezaji wao ghali zaidi kutoka Liverpool. Philippe Coutinho ametambulishwa kama mchezaji wa Barcelona kwa mara ya kwanza.

Miamba hiyo ya Catalan iliripotiwa kukubali kutoa £142 milioni kuilipa Liverpool kumleta kiungo wa Kibrazili Camp Nou, baada ya ofa kdhaa kukataliwa. Lakini Barca walifanya onesho a Coutinho Barcelona kwa namna ya kipekee kwenye video ambayo ilirushwa kupitia akaunti ya klabu ya Twitter baada ya ushindi wa Jumapili dhidi ya Levante.

Coutinho alioneshwa akitembea jukwaani akizitazama kamera, akiwapungia wapiga picha, na kuwanyosha alama ya dole gumba kwa ajili ya picha. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 sasa aliwatumia mashabiki wa klabu yake mpya kuelekea taratibu zijazo.

"Salamu Barcelona, tayari nipo hapa," alisema Coutinho. "Ni ndoto iliyotimia na natuma tutaonana kesho".

Bila ya Coutinho, Barca waliifunga 3-0 Levante na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa pengo la alama tisa, Lionel Messi, Luis Suarez na Paulinho wote wakiingia kwenye ubao wa magoli.

"Amewasili kwenye klabu ambayo daima amekuwa akiitamani," alisema mshambuliaji wa Barca, Luis Suarez, mchezaji mwenzake Coutinho wa zamani. "Nimefurahi kwa sababu nina mahusiano mazuri na Philippe. Ni budi tumfanye ajisikie yupo nyumani kwa sababu wakati mwingine ni vigumu kubadili klabu.

"Kila mmoja anafahamu kipaji alichonacho amekuwa kwenye kiwango safi ndani ya miaka michache. Ni mchezaji mahiri, asilimia 200 na amethibitisha thamani yake kama mchezaji."


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.