Bongo Fc


Man utd mbioni kutoa kiasi hiki cha mtonyo kumnasa mesut ozil..

Manchester United wana amini kuwa paundi milioni 35 zinatosha kumg'oa kiungo wa Arsenal Mesut Ozil kwa mwezi huu wa Januari.

Ozil ambaye yupo kwenye mwaka wake wa mwisho , amegoma kuongeza mkataba mpya pale Emirates na gazeti la Mirror limesema kwamba Mourinho amepewa ruksa ya kuzungumza na nyota huyo mwenye umri wa miaka 29

Gazeti hilo pia limesema kwamba Mourinho amepanga kutumia paundi milioni 80 kwa mwezi huu wa Januari, na anajiandaa kujidiliana na Gunners kuhusu bei ya kulipa kwa ajili ya nyota huyo

Wenger ana nia ya kumbakiza North London nyota huyo wa Ujerumani, licha ya Ozili kubakiza siku chache kwenye mkataba wake. Bayern Munich na Paris Saint Germain pia zimekuwa zikuwania Mesut Ozil


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.