Bongo Fc


Kwasi atangaza vita kwa ajibu, chirwa

Baada ya kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza, beki wa Simba, Asante Kwasi amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ubora wa washambuliaji Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu wa Yanga.

Kwasi amejiunga na Simba kutoka Lipuli ya Iringa katika usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka jana.

Haikuwa kazi rahisi kwa Lipuli kumpa ruksa ya kuondoka beki huyo wa kati kutokana na ubora na umuhimu wake katika kikosi hicho. Lakini, juhudi za vigogo wa Simba kuishawishi Lipuli zilizaa matunda na mchezaji huyo wa kigeni kutoka Ghana ni mali ya Wekundu wa Msimbazi.

Kwasi amedhihirisha ubora wake na Simba baada ya kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Jamhuri katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Simba ilishinda mabao 3-1. Muda mfupi baada ya kupata mafanikio hayo, beki huyo amewageukia Chirwa na Ajibu akitamba kuwa atawanyoosha.

Akizungumza hivi karibuni, Kwasi alidai kuwa Chirwa na Ajibu ni washambuliaji hodari wasumbufu, lakini dawa yao inachemka. Kwasi alisema Chirwa mwenye mabao sita na Ajibu matano ni wachezaji ni hatari wanapokuwa langoni mwa adui kwa kuwa wana kipaji cha kufunga.

“Chirwa na Ajibu nimekutana nao katika Ligi Kuu, nilicheza vizuri dhidi yao lakini kama tutakutana tena nitawapa ulinzi mkali,” alisema Kwasi.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.