Bongo Fc


Hatimaye messi aifikia rekodi ya miaka 39 ya muller kwa mabao 365 ya la liga barcelona

Mwargentina huyo asiye na mpinzani ameweka historia mpya katika mechi 27 pungufu zaidi ya mshambuliaji wa zamani wa Bayern, akiivunja rekod yake yote.

Lionel Messi ameifikia rekodi ya Gerd Muller iliyodumu kwa muda mrefu kwa kuweka kimiani magoli 365 ya La Liga kwa Barcelona.

Mkali huyo wa Kiargentina alifungua ukurasa wa magoli kwa miamba wa Catalan Jumapili kwa goli la kiufundi dhidi ya Levante.

Messi aligongeana na mchezaji mwenzake mkongwe Jordi Alba na kumalizia kwa kuukwamisha wavuni mpira kuipa goli la kuongoza 1-0 timu yake ugenini katika ushindi wa 3-0 ugenini.

Na, kwa kufanya hivyo, La Pulga alilingana magoli na supastaa wa zamani wa Bayern na Ujerumani akiifikia rekodi ambayo imedumu kwa muda wa miaka 39.

Sasa amefunga magoli 365 akiwa Blaugrana katika mechi 400 za La iga, akiifikia rekodi hiyo ya kihistoria ya Muller aliyofanikiwa kuiweka Muller kwenye klabu moja miongoni mwa Ligi Kuu tano za Ulaya.

Rekodi inaweza kuvunjika Jumapili ijayo Barca watakapoitembelea Real Sociedad. Cha zaidi, Messi aiifikia rekodi kwa mechi 27 pungufu za gwiji huyo wa Bayern Muller, ambaye alihitaji mechi 427 kufikia idadi hiyo ya magoli.

Messi tayari ameshavunja rekodi moja ya Muller mwezi Desemba, akifunga goli lake la 526 kwa Barcelona kwenye michuano yote dhidi ya Real Madrid na kuipiku idadi ya Mjerumani huyo akiwa kwenye kabu moja.

Na baada ya kiwango safi dhidi ya Levante ambacho pia kilihusishwa pasi ya goli, hakuna atakayebisha kuwa nambari 10 huyo ataendelea kuingia kwenye vitabu vya rekodi misimu ijayo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.