Bongo Fc


Azam fc yawazia fainali mapinduzi cup

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche, amesema baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, wanajipanga kuhakikisha wanatinga fainali.

Azam juzi ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwanyuka Wekundu wa Msimbazi, Simba bao 1-0, mchezo uliopigwa Dimba la Amaan, Unguja.

Azam ipo kundi A katika michuano hiyo ikiwa pamoja na Simba, URA, Mwenge na Jamhuri.

Ilifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kufikisha kushinda michezo yake mitatu na kufikisha pointi tisa, URA ikiwa katika nafasi ya pili na pointi saba, Simba kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne, Jamhuri kwenye nafasi ya tano ikiwa na pointi moja.

Akizungumza na BongoFC jana, Cheche alisema kikosi chake kinazidi kuimarika siku baada ya siku, hatua inayomfanya aamini kina fursa ya kutwaa taji hilo kwa mara nyingine.

“Baada ya kupata ushindi dhidi ya Simba, kwa sasa tunaendelea na mazoezi lengo likiwa ni kuhakikisha tunajiweka imara kabla ya mchezo wa nusu fainali.

“Kusudio letu ni lile lile kuhakikisha tunatetea ubingwa wa michuano hii,” alisema. Cheche akiwa anakaimu nafasi ya kocha mkuu wa Azam, aliiongoza kutwaa ubingwa wa michuano iliyopita ya Kombe la Mapinduzi.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.