Bongo Fc


Countinho kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu barca (+picha)

Mchezaji mpya wa klabu ya Barcelona, Philippe Coutinho atalazimika kuwa nje ya Uwanja kwa muda wa wiki tatu baada ya kufuatia kugundulika kuwa na majeraha ya nyama za paja wakati akifanyiwa vipimo vya afya na timu hiyo.

Hatua za upimaji wa afya kwa Countinho raia wa Brazili zimefanyika mara mbili kwa nyakati tofauti na kugundulika kuwa na majeraha hayo mguu wa kulia.

Coutinho atalazimika sasa kukosa mchezo ujao wa Copa del Rey dhidi ya Celta Vigo na ile ya Real Sociedad, Real Betis na Alaves. Kwa hali hiyo mchezaji huyo atashuhudiwa katika mchezo wake wa kwanza wa Catalan derby dhidi ya Espanyol.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, amefanikiwa kuweka historia katika soka baada ya usajili wake wa miaka mitano kujiunga na Barcelona wa paundi milioni 145 kuwa wa gharama na kushika nafasi ya pili baada ya ule wa Neymar kwenda PSG.
Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.