Bongo Fc


Wenger aweweseka kwa kipigo

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amewashukia wachezaji wake akidai ndio chanzo ya kupata aibu katika mchezo wa Kombe la FA.

Arsenal iliduwazwa na timu ya daraja la kwanza Nottingham Forest kwa kunyukwa mabao 4-2 juzi usiku na kutupwa nje kwenye mashindano hayo.

Matokeo hayo yamemuibua kocha huyo Mfaransa ambaye alidai uzembe wa wachezaji ulichangia kupata kipigo. Kocha huyo akionekana kuchukizwa na matokeo hayo alisema Arsenal ilishindwa kucheza vyema idara zote katika mchezo huo.

Wenger alifanya mabadiliko kwa wachezaji tisa, lakini walishindwa kucheza katika ubora ambao alitarajia. “Hatukuwa makini katika idara zote tulicheza chini ya kiwango, siyo mbele tu, hata kiungo, ulinzi na hatukuwa kwenye ubora wetu,” alisema Wenger.

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Monaco aligoma kuzungumzia penalti mbili za wapinzani wao. “Najua uamuzi wangu wa kupanga timu utaibua maswali mengi, lakini tulikuwa na wachezaji wanane hadi tisa wenye uzoefu wa kimataifa,”alisema Wenger.

Alisema anaipongeza Nottingham Forest kwa ushindi na ameridhishwa na kiwango cha uchezaji wao katika mchezo huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kushindwa kupenya katika raundi ya nne ya Kombe la FA, lakini Nottingaham Forest ni timu ya kwanza ya ‘mchangani’ kupata mabao manne tangu Januari 1908 ilipochapwa na Hull City.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.