Bongo Fc


Tambwe kuikosa nusu fainali

Wakati timu yake ikitinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar, mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe ana hatihati ya kuukosa mchezo wa hatua hiyo baada ya kurejeshwa Dar kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua Maralia.

Tambwe jana mchana alipanda boti kurejea Dar es Salaam wakati kikosi chake kikijiandaa kuvaana na Singida United kwenye mchezo wa mwisho hatua ya makundi.

Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, alisema kuwa Tambwe amelazimika kuondoka kwenye kambi ya timu hiyomjini Zanzibar ili arejee jijini kupata matibabu. “Kwa siku nne sasa amekuwa na Maralia, tumeona ni vyema arejee Dar es Salaam ili kujitibu na kupata matibabu kamili,” alisema Bavu.

Tambwe, amekuwa na wakati mgumu msimu huu akiandamwa na majeraha na kuondoka kwake Zanzibar kunamaanisha ataukosa mchezo wa hatua ya nusu fainali unaotazamiwa kuchezwa kesho Jumatano.

Yanga sasa itamtegemea zaidi mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu kwenye safu ya ushambuliaji. Ajibu na Tambwe ndio washambuliaji wenye uzoefu kwenye kikosi hicho katika mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.