Bongo Fc


Marcelo adai ni huzuni kwamba real imezama..

Beki huyo hakuweza hata kutumia tafsida baada ya kuishuhudia timu yake ikilazimishwa na sare dhidi ya Celta.

Marcelo amekiri kuwa Real Madrid wana huzuni nyingi baada ya kuachwa pointi 16 na Barcelona inayoongaza msimamo wa La Liga. Mabingwa watetezi Madrid msimu wao umeendelea kuwa mbaya zaidi baada ya kushikiliwa kwa sare ya 2-2 dhidi ya Celta Vigo.

Gareth Bale alifunga mara mbili kusawazisha goli la Dniel Wass na kuipa Madrid goli la kuongoza kabla ya mapumziko. Lakini bado hali haikuwa nzuri kwa Madrid kwani Celta walisawazisha dakika ya 82 kupitia Maxi Gomez baada ya penalti ya Iago Aspas kuokolewa dakika 10 kabla.

"Tuna huzuni kwani tumezama, alisema Marcelo baada ya mchezo. "Tunajaribu kujitoa kwenye fedheha hii, na tunajitahidi kufanya hivyo kwa sababu hatuipendi hii hali.

"Ni vigumu kwa sababu kadiri unavyotoa sare nyingi au kupoteza ndivyo presha inavyoongezeka. Hatuwezi kufanya chochote. "Tunafanya kile tunachoweza, tunajitahidi kucheza soka zuri na kuutembeza mpira, lakini mambo hayatuendei vizuri."

Madrid, ambao hawajashinda mechi nne za ugenini La Liga, wanashika nafasi ya nne kwenye ligi, nyuma ya Atletico Madrid na Valencia.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.