Bongo Fc


Simba yachemsha kombe la mapinduzi

Licha ya kumiliki mpira kwa zaidi ya asilimia 56, Simba inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa jana ilishindwa kupata ushindi mbele ya URA na kukubali kipigo cha bao 1-0 kilichowatupa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho inayoendelea visiwani Zanzibar.

Simba ilijikuta ikimaliza michezo yake ya hatua ya makundi kwa kufikisha pointi nne tu huku ikiachwa kwa pointi sita na vinara URA na pointi tano na Azam FC zilizofuzu hatua ya nusu fainali.

Kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Azam ambao Simba walilala kwa kipigo kama cha jana, Simba iliendelea kutokuwa makini kwenye safu yake ya ulinzi na kupelekea kuruhusu bao hilo pekee lililofungwa na Deboss Kalama kwa shuti baada ya kuwatoka mabeki wa Simba katika dakika ya tano za nyongeza baada ya dakika 45.

Simba ambayo kwenye mchezo wa jana iliendelea kutumia mfumo wa 3-5-2 ambao bado haujaonekana kuwaingia wachezaji hususani safu ya ulinzi na mawinga.

Simba ambayo kwenye mchezo wa jana ilikuwa ikihitaji ushindi tu kuweza kusonga mbele, itabidi ijilaumu yenyewe kutokana na umakini mdogo wa safu yake ya ushambuliaji iliyokuwa ikioongozwa na nahodha John Bocco.

Bocco ndiye aliyeongoza kwa kukosa magoli mengi, kwani dakika ya 15 alipiga kichwa lakini kiliokolewa kwa ustadi mkali na kipa wa URA, Alionzi Nafian ambaye alikuwa nyota wa mchezo.

Kipindi cha pili, URA iliyokuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu hatua ya nusu fainali ilibadili mfumo na kucheza zaidi mchezo wa kujihami, lakini ikishambulia kwa kushtukiza, huku mashambulizi yao yakiwa makali na ya hatari kwa wapinzani wao.

Kocha Masoud Djuma licha ya kuwatoa Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto na Nicolaus Gyan kipindi cha pili na kuwaingiza Yusuph Mlipili, Laudit Mavugo, James Kotei na Mohamed Ibrahim, ambao walijitahidi kwa kila hali angalau hata kurudisha bao, lakini uimara wa safu ya ulinzi ya URA iliwanyima bao.

Kwa matokeo ya jana, URA imetinga hatua ya nusu fainali kama vinara wa kundi A pamoja na Azam walioshika nafasi ya pili, timu hizo zitaumana na Yanga au Singida United kwenye hatua hiyo ya nusu fainali.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.