Bongo Fc


Spurs itamlazimisha harry kane kubaki, akiri pochettino

Mshambuliaji huyo mwenye kasi ya ajabu ya kucheka na nyavu ameiwezesha Spurs kusonga mbele Kombe la FA na mataji yatamshawishi kubaki klabuni. Mauricio Pochettino amesema kuwa kupata mataji kutamshawishi Harry Kane kuendelea kubaki.

Mabao mawili ya Kane yalikuwa muhimu kwa Spurs kushinda 3-0 dhidi ya AFC Wimbledon raundi ya tatu Kombe la FA Jumapili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hakutarajiwa kucheza katika uwanja wa Wembley, lakini alikuwa nahodha wa Spurs na kufunga mara mbili katika muda wa tofauti ya sekunde 111 baada ya wapinzani wao wa League One kugonga besela mapema.

Kama ilivyo kwa timu nyingine za Premier League, Spurs imeshindwa kuifukuzia Manchester City, kwa hiyo kwenda mbali zaidi Kombe la FA kuliko msimu uliopita itawasaidia kumshikilia vizuri Kane.

"Nadhani Harry Kane ni wa kipekee. Anaipenda Tottenham," Pochettino alisema akimzungumzia mchezaji huyo aliyefunga magoli 56 mwaka 2017. "Tunahitaji kuwa makini namna tunavyomsimamia. Kisha mchezaji atahitaji kuamua kubaki hapa. Huwezi kumlazimisha yeyote kubaki.

"Kazi yetu ni kujitahidi kwa pamoja kufanya kazi na kupata kile tunachoktaka. Naam, Harry Kane ni mchezaji mahususi. Ni kama [gwiji wa Roma, Francesco Totti]. Aliongeza, "Wachezaji wachache wanaweza kubaki kwenye klabu moja maisha yao yote na Kane anaweza kuwa mmoja wao. Lakini katika soka hakuna chenye uhakika.

"Leo ni leo na baada ya kesho unapata hofu nini kitatokea. Kwa hiyo ni muhimu tupate mafanikio tunayoyataka kwa pamoja."


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.