Bongo Fc


Kocha simba akubali yaishe!

Kocha mkuu wa Simba, Mrundi Masoud Djuma amesema, wanatamani kusonga mbele hatua ya fainali, lakini ndiyo kama hivyo Mungu hajapenda, wameondolewa.

Djuma ambaye amekabiziwa mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Mcameroon Joseph Omog, akiwa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ameshindwa kutamba na kujikuta akiaga hatua ya makundi kwa kufungwa mechi mbili, sare mmoja na ushindi mmoja.

"Tumeondolewa kwenye mashindano hayo na sasa tunawekeza nguvu zetu katika mechi za ligi kuu na michuano ya Kimataifa ambayo ndio nafasi yetu iliyobaki msimu huu," anasema Djuma ambaye kikosi chake kitaiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirikisho.”

"Tumejifunza mengi katika mashindano hayo na tumeyachukua kama changamoto kwetu ili kuweza kujirekebisha na kufanya vizuri kwenye mashindano yaliyobaki."


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.