Bongo Fc


Wanawake saudi arabia kuanza kushuhudia soka

Wanawake nchini Saudi Arabia, wataruhusiwa kuanza mwezi huu kuhudhuria kwenye michezo ya kandanda ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa maofisa wa Saudi Arabia, mashabiki wa kandanda wanawake wataruhusiwa kuingia katika viwanja vikubwa vya mpira katika taifa hilo la kifalme kuangalia michezo mitatu inayohusisha timu za kandanda zinazoshiriki ligi ya nchi hiyo.

Mechi hizo zimepangwa kuchezwa Ijumaa, Jumamosi na Januari 18.

Oktoba mwaka jana idara inayohusika na masuala ya michezo ya Saudi Arabia, ilitangaza kuwa kufikia mwaka 2018 viwanja vitatu ambavyo hadi sasa vinatumika kwa wanaume tu vitaandaliwa kwa ajili ya kutumiwa pia na familia ikiwa ni pamoja na kuwa na maeneo maalumu ya kukaa.

Mwana wa mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, inaelezwa kuwa ameondoa marufuku dhidi ya wanawake kujihusisha na mchezo wa kandanda, wakati akijaribu kurejesha kile kinachoitwa heshima ya nchi hiyo kimataifa.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.