Bongo Fc


Benitez akunjua makucha newcastle united

Kocha wa Newcastle United, Rafael Benitez amewataka mabosi wa klabu hiyo ya St James Park kununua wachezaji wapya.

Benitez ana amini timu hiyo inaweza kutoa upinzani katika mashindano ya Ligi Kuu England ikiwa na wachezaji bora.

Hata hivyo, kocha huyo Mhispania alisema anashangazwa na ukimya wa mmiliki wa klabu hiyo kuhusu usajili wakati dirisha dogo la usajili limefunguliwa lakini hakuna bajeti.

Benitez alidokeza Newcastle United inatakiwa kuuza na kununua wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi hicho.

Benitez alisema ametoa taarifa ya kutaka kusaka upya kikosi hicho na alitarajia katika dirisha la usajili kupata sura mpya.

Kocha huyo wa zamani wa Liverpool alisema hawezi kumpiga bei mchezaji yeyote kabla ya kupata saini ya mchezaji mpya na kumuweka sokoni mchezaji majeruhi Aleksandar Mitrovic.

Pia Benitez anapambana kumbakiza St James Park kiungo mtukutu Jonjo Shelvey, aliyetupiwa ndoano na klabu ya West Ham United.

Mchezaji huyo mwenye miaka 25, amekuwa akiandamwa na matukio ya utovu wa nidhamu ndani ya uwanja.

Newcastle United inataka kujijenga katika usajili wa dirisha dogo baada ya kushindwa kutamba msimu huu ikikabiliwa na janga la kuteremka daraja.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.