Bongo Fc


Yanga yashtukia ‘janja’ ya ura

Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa kwenye mchezo wa leo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi watakuwa makini baada ya kugundua mbinu za wapinzani wao URA.

Nsajigwa, alisema kuwa watahakikisha wanakuwa makini kwenye safu yao ya ulinzi na viungo hasa kutokana na URA kutumia mfumo wa kujihami na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

“Tumewaona kwenye mchezo wao dhidi ya Simba, ni timu nzuri yenye wachezaji wepesi, tutakabiliana nao kwa umakini mkubwa, ili tuweze kusonga mbele,” alisema Nsajigwa.

Alisema kuwa wanafahamu URA watakuja na mtindo wa kujihami huku wakitegemea mashambulizi ya kushtukiza kuwaadhibu, lakini watakuwa makini na hilo.

Wakati Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa ikiingia kwenye hatua hiyo baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi B nyuma ya Singida United, URA wenyewe wametinga hatua hiyo baada ya kuongoza kundi A mbele ya Azam FC ambao nao wataumana na Singida United kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa usiku.

Timu hiyo kutoka Uganda, imeonekana kuwa na nidhamu kubwa kwenye kujilinda huku wakiwa wazuri kwenye mashambulizi ya kushtukiza.

Kwenye mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Simba ambao walikuwa wakihitazi sare kutinga nusu fainali, URA ilifanikiwa kuwabana Simba na kupata ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo wa leo utakaoanza majira ya saa 10:00 jioni, Yanga wanapaswa kuwa makini katika safu yao ya ulinzi kuhimili mshambulizi ya kushtukiza ya Waganda hao.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.