Bongo Fc


Azam fc yawatoa hofu mashabiki

Ikiwa leo ndio nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar, kocha msaidizi wa Azam FC Idd Cheche amesema mashabiki waondoe hofu kwani watatetea ubingwa wao.

Azam FC ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo na wametinga nusu fainali wakitokea kundi B kwa kushika nafasi ya pili nyuma ya URA ya Uganda.

''Kuhusu kutetea ubingwa wetu mashabiki wasitie shaka, tumekuja kwa dhamira moja tu na tuko pamoja tumeungana kupambana kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu'', amesema Cheche.

Azam FC itakuwa kibaruani dhidi ya Singida United ambayo nayo imetinga nusu fainali kwa kuongoza kundi A. Mchezo huo utachezwa majira ya saa 2:00 usiku.

Kuhusu mchezo wa leo kocha Cheche amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda huku akikiri kuwa hatua ya nusu fainali itakuwa ngumu tofauti na ilivyokuwa hatua ya makundi.

Msimu huu Azam FC na Singida United zimekutana mara moja kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo timu hizo zilitoka sare.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.