Bongo Fc


Gerrard amtumia ujumbe mzito coutinho

Ikiwa ni takribani siku moja sasa baada ya kiungo wa Brazil Philippe Coutinho kusaini mkataba wa kuichezea klabu ya Barcelona akitokea Liverpool, nahodha wa zamani wa timu hiyo Steven Gerrard amemwandikia ujumbemzito nyota huyo.

Gerrard ambaye alicheza pamoja na Coutinho ndani ya Liverpool amesema inaumiza sana kwa klabu kumpoteza mchezaji wa kiwango cha juu kama Coutinho lakini pia amemtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya ndani ya Barcelona.

Coutinho alimkuta Gerrard akiwa nahodha wa Liverpool wakati amesajliwa kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia mwaka 2013 kabla ya Gerrard kuondoka klabuni hapo mwaka 2015 na kutimkia katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani.

Coutinho ameichezea Liverpool michezo 152 na kuifungia mabao 41, katika misimu mitano na nusu. Hata hivyo Coutinho atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu kutokana na maumivu ya paja yanayomsumbua.

''Kuondoka kwako kunaumiza sana kwasababu wewe ni mchezaji muhimu kutokana na tulivyoshirikiana uwanjani, nakutakia kila la kheri wewe na familia yako kwenye maisha yako mapya ndani ya Barcelona. Asante kwa kumbukumbu zote nzuri katika miaka yako mitano ndani ya Liverpool'', ameandika Gerrard.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.