Bongo Fc


Kocha simba ampiga biti kwasi

Benchi la ufundi la Simba chini ya kaimu kocha wake mkuu, Masoud Djuma, raia wa Burundi, limempa tahadhari beki mpya wa timu hiyo, Asante Kwasi, raia wa Ghana, kwamba anatakiwa kuendelea kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kuendelea kusalia katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Kwasi alijiunga hivi karibuni na Simba katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Desemba 15, mwaka jana akitokea Lipuli FC ya Iringa kwa dau la milioni 25, ambapo tayari ameshatumika katika mechi mbili za timu hiyo katika Kombe la Mapinduzi.

Kwa muibu wa Gazeti la Championi Jumatano, Mrundi huyo ameliambia gazeti hilo kuwa Mghana huyo asijiamin­ishe kwamba ana namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho kutokana na yeye kubadili kikosi chake kutokana na mahitaji ya mechi husika lakini pia ushindani wa namba uliopo baina ya wachezaji wake. Imeelezwa.

“Ingawa kwa sasa tunamtu­mia zaidi Kwasi katika kikosi cha kwanza lakini siyo kwamba ndiyo ana namba ya kudumu katika timu hiyo, kwangu ninaangalia aina ya mechi na mahitaji ya watu ambao ninawataka, hivyo ninaweza kupangua baadhi ya watu kutokana tu na aina ya mpinzani ambaye tunakabiliana naye.

“Lakini pia inabidi yeye aendelee kuonyesha kiwango kwani kama unavyojua hapa kuna wachezaji wengi wenye uwezo, sasa ni lazima kwamba ili uendelee kudumu katika kikosi cha kwanza, ni lazima uonyeshe uwezo mkubwa zaidi ya wenzako,” alisema Djuma.

Simba ina mabeki sita wa kati ambao ni Kwasi, Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Salum Mbonde, Paul Bukaba na kiraka Erasto Nyoni.

Chanzo: Championi Juma5


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.