Bongo Fc


Lukaku akasirishwa na tuhuma za ushirikina, akimbilia mahakamani

Moja kati ya habari kubwa duniani siku ya jana ni kumhusu Romelu Lukaku, baada ya moja ya wakurugenzi wa Everton kudai mwanasoka huyo alitumiwa ujumbe na mganga wa kienyeji ahame Everton.

Farhadi Moshiri alidai kwamba mshambuliaji huyo hakuondoka Everton kwa sababu za kifedha wala mshahara lakini Lukaku aliondoka Everton kwa sababu ya ushauri wa masuala ya kishirikina.

Habari hizi zimemfikia Romelu Lukaku na watu wake wa karibu wanasema amekasirishwa sana na jambo hilo, tayari Romelu Lukaku ameanza kutafuta ushauri wa kisheria ili kumchukulia hatua Moshiri.

Mwakilishi wa mchezaji huyo aliiambia BBC Sport kwamba, "Uamuzi wa Lukaku haukushinikizwa na uchawi". Msemaji huyo aliongezea, "Hapendi kufuata imani kama hizo na sasa anatathmini hatua za kisheria anazoweza kuchukua".

Wawakilishi wake wanasema kuwa Lukaku alikataa kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika historia ya klabu ya Everton ili kuweza kucheza katika klabu kubwa duniani.

Wawakilishi wake waliongezea, "Romelu ni mfuasi wa kanisa katoliki na kwamba haamini uchawi. Hakuwa na imani na Everton mbali na mradi wa bwana Moshiri".

"Hiyo ndio sababu hakutaka kutia kandarasi nyengine". Alimalizia mwakilishi wa mchezaji huyo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.