Bongo Fc


Francis coquelin wa arsenal akubali kutua valencia kwa £10.5m

Kiungo wa Arsenal Francis Coquelin ameripotiwa kuwa amekubali kuhamia Valencia. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vimedai kuwa benchi limemchosha mchezaji huyo wa Kifaransa na sasa ameamua kutimkia Hispania.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mekuwa mchezaji wa miamba hiyo ya London tangu 2008 alipojiunga na akademi ya vijana.

Katika misimu ya hivi karibuni, kiungo huyo ameshuka na kukosa namba kikosi cha kwanza akiwa nyuma ya Granit Xhaka, Mohamed Elneny na Jack Wilshere.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Coquelin sasa ameamua kuachana na Arsenal kwa kujiunga na Valencia kwa kiasi kinachokadiriwa kuwa £10.5m.

Klabu nyingine za Uingereza ikiwa ni pamoja na West Ham United, zilitarajiwa kuvutiwa kumsajili Mfaransa huyo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.