Bongo Fc


Xavi: real madrid hawataki kucheza soka la kuvutia

Legendari wa Barcelona Xavi ameukosoa mfumo wa uchezaji wa Real Madrid kwa kudai kuwa kwa miaka mingi hauna mvuto.

Mchezaji aliyeitumikia miaka mingi Barcelona yenye umaarufu Xavi ameisifia klabu yake ya zamani kuwa ilishinda mataji yasiyohesabika kati ya 2008 na 2011, sambamba na Jose Mourinho kutua Bernabeu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal amedai kuwa Real hawataki kucheza "soka la kuvutia", akiishutumu Los Blancos kwa kushambulia moja kwa moja nyavu za wapinzani wao.

"Barcelona ni mtihani wa mwisho kwa mchezaji," aliiambia El Pais. "Ni klabu ngumu sana na inayotaka mengi duniani. Madrid hawachezi soka la kuvutia. Katika Bernebeu, kama beki akibutua mpira ni sawa. Huu ni utamaduni wao. Wachezaji watapiga makofi.

"Lakini Camp Nou ukiupiga mpira ukaenda nje, umati utapiga kelele na kuzomea. Tangu nyakati za [Johan] Cruyff. Madrid ya Mourinho ilikuwa ikipiga mipira ya moja kwa moja kuelekea golini tu. Mourinho aliwaambia wachezaji wake wasitulize mpira, wacheze kwa haraka na [Angel] Di Maria, Cristiano [Ronaldo] au [Karim] Benzema angeshambulia.

"Na sasa wanafanya hivyo na [Gareth] Bale. Real hawataki kucheza mpira. Madrid inasambaratika, wachezaji saba wanashambulia na Casemiro anabaki nyuma peke yake. [Sergio] Busquets hawezi kufanya hivyo kwani hata mimi nina kasi kuliko yeye. Casemiro ana kasi zaidi, lakini anapata matatizo mengi ambayo hajayafanyia kazi.

"Anazo sifa nyingine, ni mkabaji mzuri, anawavaa vizuri wapinzani, anaziba vizuri uwanja, lakini hawezi kutumia vizuri muda na nafasi. Kama ungeanza na Casemiro akiwa na umri wa miaka 12, 13, 15 angekuwa na sifa zote."

Xavi sasa anaichezea Al Sadd ya Qatari, baada ya kustaafu soka Barcelona 2015.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.