Bongo Fc


Kocha azam: azam bingwa kombe la mapinduzi

Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema anauhakika timu yake itatetea ubingwa wake wa Kombe la Mapinduzi kutokana na ari waliyokuwa nao wachezaji wake.

Coaba ameiambia BongoFC, anajua anakwenda kukutana na URA timu ambayo iliwafunga kwenye mchezo wa makundi hivyo walichopanga ni kulipa kisasi na kutwaa ubingwa wao kama ilivyokuwa mwaka jana.

"Siwezi kuwaogopa URA wala kuwazarau lakini ninachojua Azam itateakombe lake, kwasababu hatutokubali kufungwa mara mbili na timu moja mechi hiyo tumeipa uzito na tulichopanga ni kulipa kisasi na kuchukua kombe letu,"amesema Cioaba.

Kocha huyo hakusita kuwasifia wachezaji wake kwa mapambano waliyoonyesha kwenye mchezo huo wa nusu fainali dhidi ya Singida United na kusema kitu hicho ndiyo kinampa matumaini ya kusema hivyo.

Fainali ya michuano hiyo imepangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja huo wa Amaan majira ya saa 2:15 usiku ambapo ndipo bingwa wa 12 wa michuano hiyo atakapo julikana.

Azam ilitinga fainali jana usiku baada ya kuwafunga Singida United bao 1-0, na kuiweka timu hiyo ya tajiri Salim Said Bakressa katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake kwa mara ya pili.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.