Bongo Fc


Cheki mkeka wa owen mechi za epl

Na: Omary Ramsey

Nyota wa zamani wa Liverpool, Michael Owen ameweka utabiri wake kuhusu mechi za Ligi Kuu England zitakazopigwa Jumapili hii, huku akidai kwamba kipute cha Liverpool na Manchester City kitamalizika kwa sare huko Anfield.

Mechi hiyo kubwa itapigwa leo Jumapili na Owen anadai kwamba timu hizo zitatoka sare ya 2-2, huku akidai Arsenal watakaokuwa ugenini kwa Bournemouth, Owen amesema kwamba Arsene Wenger na timu yake itashinda 2-1.

Manchester United watakaocheza Jumatatu, wametabiriwa kuishinda Stoke City huko Old Trafford licha ya kukiri kwamba Stoke wamekuwa na rekodi ya kutopoteza mechi yoyote ya ugenini waliocheza Jumatatu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.