Bongo Fc


Pluijm akubali mziki wa simba

Kocha wa Singida United, Hans Van Pluijm, amekiri kikosi chake kilikuwa na mapungufu hasa katika safu ya ulinzi ndiyo maana walikumbwa na kipigo cha aibu cha mabao 4-0 mbele ya Simba juzi Alhamisi.

Pluijm alisema kufanya makosa mengi mbele ya timu kubwa kama Simba ndio kilichochangia kufungwa magoli mengi, lakini wamejifunza kitu.

“Simba walikuwa bora zaidi yetu katika mechi hii na kama watakuwa wanacheza kama hivi katika mechi zinazokuja, watafanya vizuri zaidi ya hapa,” alisema Pluijm.

“Simba ina wachezaji makini na wazoefu na hili linaweza kuwa shida au faida kwao pale wanapokutana na wachezaji ambao hawana uzoefu wa ligi,” alisema Pluijm ambaye tangu ameanza kufundisha soka nchini hajawahi kufungwa mabao zaidi ya mawili.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.