Bongo Fc


Sturridge atua kwa mkopo west bromwich albion

Mshambuliaji Daniel Sturridge akiwa amevaa jezi ya West Bromwich Albion baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Liverpool.

Sturridge amejiunga na timu hiyo baada ya kuonekana kukosa namba katika kikosi cha Liverpool tangu alipowasili kocha Jürgen Klopp mwaka 2015.Baada ya kufanikiwa kukamilisha uhamisho wake huo wa mkopo na kukabidhiwa jezi yake yenye namba 15 ambayo amezoea kuivaa, mchezaji huyo amesema, “Nilifahamu hii itakuwa klabu sahihi kwangu. Nina marafiki hapa nilicheza nao kabla, meneja alizungumza vizuri na kuna changamoto ya timu na mtindo wa kucheza.”

Awali mchezaji huyo alikuwa anawaniwa na timu kadhaa ikiwemo Newcastle United.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.