Bongo Fc


Fahamu wanasoka waliotoka kimapenzi na waandishi wa habari.. orodha kamili hii hapa

Na: Omary Ramsey

Kama walivyo wanamichezo wengine, wanasoka nao wamekuwa karibu na waandishi wa habari katika utendaji kazi wao. Hata hivyo, ukaribu huo wa kikazi umesababisha mara kadhaa kusikia wanasoka wakijikuta wakiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na waandishi wa kike.

Ni kama ilivyotokea kwa wachezaji hawa, ambao waliwahi kutoka na waandishi, hata wengine kufikia hatua ya kufunga ndoa.

(01) Prince Boateng (Melissa Satta)

Huyo ni kiungo mwenye asili ya Ghana ambaye kwa sasa anakipiga Bundesliga katika klabu ya Frankfurt. Baada ya kuachana na bibiye Jenny, Boateng aliangukia kwenye penzi la mwandishi wa habari aitwaye Melissa Satta ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kituo cha televisheni cha TIM.

Boateng alikutana na Satta mwaka 2011 na wawili hao walioana mwaka 2016 na wameshabahatika kupata mtoto mmoja.

Kwa mashabiki wa soka, watakumbuka kuwa Satta ndiye mwanamke aliyedai kuwa kuumia mara kwa mara kwa Boateng kulitokana na alikuwa akifanya mapenzi mara saba au 10 kwa wiki.

(02) Sergio Ramos (Pilar Rubio)

Kwa mashabiki wa Real Madrid, huyo ni zaidi ya nahodha kutokana na aina yake ya uchezaji wa ‘jihad’. Kwa upande wa pili, anayempoza machungu pale mambo yanapokuwa hayaendi sawa uwanjani ni mwandishi, Pilar Rubio. Ndiye mkewe.

Rubio ni mtangazaji wa kituo cha televisheni cha La Sexta cha Hispania. Wawili hao walianza kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi mwaka 2012 na tayari wana watoto wawili (Sergio na Marco).

Kwa wafuatiliaji wa habari za mastaa, watakumbuka kuwa Pilar ndiye aliyetajwa kuwa mwanamke mwenye mvuto zaidi Hispania kwa mwaka 2008 na akaibeba tena tuzo hiyo mwaka 2009. Ni tuzo ambayo hutolewa na jarida la FHM la nchini humo.

(03) Iker Casilas

Umaarufu wake mkubwa ulitokana na umahiri wake langoni mwa Real Madrid kabla ya kutimkia Porto ya Ureno anayoichezea hadi sasa. Casillas ni mume wa Sara Carbonero, mwandishi wa habari maarufu nchini Hispania. Mapenzi yao yalianza mwaka 2009, kipindi ambacho Casillas alikuwa na kikosi cha Madrid.

Walipata mtoto wao wa kwanza aitwaye Martin mwaka 2014. Kilichofuata ni ndoa iliyofungwa mwaka 2016, kabla ya ujio wa mwingine wanayemwita Lucas.

(04) Ronaldo (Lucia Villalon)

Georgina Rodriguez ndiye mpenzi wake wa sasa, lakini kabla ya hapo Cristiano Ronaldo, aliwahi kuwa na mwandishi wa Hispania, Lucia Villalon.

Taarifa za mwanasoka huyo kutoka na Lucia ziliibuka wiki chache baada ya kubwagana na mwanamitindo wa Urusi, Irina Shayk. Tetesi hizo zilipata kasi baada ya wawili hao kunaswa wakisherehekea tuzo ya tatu ya Ballon d’Or aliyokuwa ameshinda nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno.

(05) Alessandro Matri (Federica Nargi)

Huyo ni straika wa Sassuolo ya Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’. Aliwahi pia kucheza Juventus. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia anatoka na mwandishi mwenye jina kubwa Italia, Federica Nargihave, ambaye alianza kuwa naye tangu mwaka 2009.

Mapenzi yao hayakuanza jana, tangu wakiwa na umri wa miaka 17. Mrembo Nargihas, amekuwa mtangazaji kwa miaka mingi licha ya kwamba ndiyo kwanza ana umri wa miaka 25 kwa sasa.

(06) Wayne Rooney (Coleen Rooney)

Mbali na kazi yake ya uanamitindo, mke wa staa wa Everton, Wayne Rooney, Coleen, ni mwandishi wa habari. Mama huyo wa watoto watatu (sasa mjamzito), alikuwa mtangazaji na mwenye jina jijini Liverpool na pia mwandishi wa kolamu za mitindo.

Wawili hao walianza kutoka kimapenzi wakiwa na umri wa miaka 16 na walifunga ndoa mwaka 2008.

(07) Rafael van der Vaart (Sylvie Meis)

Mmoja kati ya viungo bora kuwahi kutokea katika soka la Ulaya. Hivi sasa anaichezea Midtjylland ya Denmark. Naye aliwahi kutoka na mwandishi wa habari aitwaye Sylvie Meis, lakini wameshaachana na sasa anajiachia na mlimbwende, Estavana Polman.

Tukirudi kwa Sylvie, bibiye alitamani uanamitindo lakini aliangukia kazi ya uandishi wa habari katika kituo cha televishebi cha Foxkids and Music Station (TMF). Alianza kutajwa kutoka na Van der Vaart mwaka 2003 na walibahatika kupata mtoto mmoja.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.