Bongo Fc


Ozil naye akubaliana na arsenal hadi juni 2021

Winga wa Ujerumani Mesut Ozil amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu kuendelea kubaki Arsenal mpaka mwezi Juni 2021.

Mkataba huo mpya unamfanya Ozil sasa kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya klabu hiyo kiasi cha £ 350,000 (Bilioni 979) kwa wiki kabla ya kukatwa kodi.

Jana ilikuwa ni siku nzuri kwa Arsenal ikiwa imetoka kukamilisha usajili wa Pierre Aubameyang kutoka Borrusia Dortmund. Mkataba wa awali wa ozil ulikuwa unamalizika mwezi juni mwishoni wa msimu huu.

Ozil mwenye miaka 29 alijiunga na washika mitutu hao wa jiji la London mwaka 2013 akitokea klabu ya Real Madrid kwa dau la rekodi ya klabu £ 42.4m (Bilioni 119) ambayo jana imevunjwa na usajili wa Aubameyang kwa dau la £ 56 (Bilioni 156).


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.