Bongo Fc


Aubameyang afuata nyayo za henry, arsenal

Mchezaji Pierre-Emerick Aubameyang anahitaji kufuata nyayo za legendari wa timu hiyo Thierry Henry baada ya kukabidhiwa jezi namba 14 ndani ya klabu ya Arsenal.

Aubameyang atakuwa akivaa jezi namba 14 ndani ya Emirates baada ya kukamilisha usajili uliyoweka rekodi ya klabu hiyo wa paundi milioni 56 akitokea Borussia Dortmund.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema kuwa Arsenal inahistoria kubwa nyuma yake huku akiamini kuwa atamthitishia hilo straika wazamani wa timu hiyo Henry.

“Kabla ya yote nijiskia furaha kuwa hapa, na bila shaka naungana na Henrikh Mkhitaryan,” amesema Aubameyang kupitia tovuti ya timu hiyo.

Alipoulizwa sababu ya kuichagua Arsenal, Aubameyang amesema “Klabu hii ina historia bora kwa mastraika kama Thierry Henry huu ni mfano mzuri kwetu.”

Mchezaji huyo wazamani wa Dortmund, Aubameyang na Mkhitaryan kwa pamoja wanaunda umoja ndani ya Arsenal baada ya wote hawa kukamilisha usajili dirisha hili la mwezi Januari.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.