Bongo Fc


Kauli dhidi ya wachezaji wa afrika yamponza mkurugenzi wa michezo london

Klabu ya West Ham United imemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wachezaji Tony Henry kufuatia tuhuma za kutoa kauli ya kuwa Klabu hiyo haitaweza kusajili tena Mchezaji yoyote wa Kiafrika kauli iliyotafsiriwa kuwa inaashiria ubaguzi wa rangi.

Kwa Mujibu wa Gazeti la Daily Mail, limesema kuwa, Mkurugenzi huyo alitoa kauli kuwa Wachezaji wa Kiafrika wanasababisha ‘Ghasia’ wasipokuwepo kwenye Timu.Klabu hiyo imetoa tamko hii leo la kumsimamisha na kufanyia uchunguzi tukio hilo ambalo linaonekana limebeba Ubaguzi wa rangi kwa kuwabagua Wachezaji wa kiafrika na hatua zitachukuliwa kama atabainika ni kweli amekusudia kufanya hivyo.

West Ham ilikuwa na Wachezaji wengi wanaotoka Afrika ambao miongoni mwao wameenda timu mbalimbali akiwemo Diafra Sakho aliyejiunga na Rennes ya Ufaransa huku Andrew Ayew kutoka Ghana akijiunga na Timu yake ya zamani ya Swansea.

West Ham wanashika nafasi ya 12 katika Ligi kuu nchini England wakiwa na Alama nne zaidi ya timu inayoshika Mkia


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.