Bongo Fc


Gerard pique aiokoa barcelona mbele ya mahasimu wao

Beki wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique ameinusuru klabu yake kwa kuipatia goli la kusawazisha dhidi ya mahasimu wao klabu ya Espanyol.

Mchezo huo ambao ulitawaliwa na vurugu huku uwanja ukiwa umejaa maji kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, Barcelona walionekana kupotea hadi alipoingia mshambuliaji tegemezi wa klabu hiyo, Lionel Messi kunako kipindi cha pili.

Pique ametupia goli hilo kwa kichwa kutoka kwenye faulo ilipigwa na Messi baada ya Beki Umtiti kufanyiwa madhambi na Sergio Garcia. Barcelona bado mpaka sasa wanaongoza ligi kuu nchini Hispania kwa alama 58 na kuwa ndiyo timu ya kwanza barani Ulaya kwenye Ligi kubwa tano ambayo haijapoteza hata mchezo mmoja.

Klabu ya Atletico Madrid inashika nafasi ya pili kwa alama 46 ikifuatiwa na Valencia yenye alama 40 kwenye msimamo wa La Liga.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.